Glossary

Cash on the Bag (COB). Fedha zinazotolewa kwa wanabiashara ili kuwawezesha kulipa wakulima mapema wakati wa ukusanyaji. COB hupunguza pengo kati ya ununuzi wa mazao kutoka kwa wakulima na kupokea kwa malipo kutoka kwa wanunuzi.

Mratibu. Mtu amabaye anawajibu wa kuratibu kazi ya mawakala katika mpango wa kitabu wazi. Kwa ujumla, lakini si mara zote, mtu huyu ni mmiliki wa biashara.

Gharama za Kati. Gharama zilizotumika kwa mtandao katika kupata mazao kutoka kwa wakulima mpaka kwa mnunuzi, ambayo hukatwa kutoka kwa bei ya mnunuzi ili kupiga hesabu ya bei kwa wakulima (bei muuzaji) . Gharama hizi ni kama upakuzi, upakiaji, ada, usafirishaji na ada mpakani na ushuru.

Networks (pia inajulikana kama mitandao ya mfanyabiashara). Inafanya kazi kwa njia ya mtandao ya mawakala (wafanyabiashara), kwa kawaida kujiajiri, na kutafuta mazao ya kilimo kutoka kwa wakulima wadogo wadogo kwa niaba ya wanunuzi.

Salesforce. Teknolojia ambayo Techfortrade inatumia katika maendeleo ya kusaidia usimamizi na ufuatiliaji wa mikataba. Kwa kufanya kazi na Salesforce Foundation, tumechukulia mfumo huu wa mtandao wa internet kama jukwaa hasa ya thamani ya juu katika biashara ya kilimo. Jukwaa hili ambalo ni imara, ni bora kwa ajili ya kurekodi data kwa kila mpango , na utangamano kwa ajili ya malipo kupitia simu ya mkono.

Wafanyabiashara na mawakala. Kwa kawaida wafanyabiashara wa kujiajiri ambao hutafuta mazao kutoka kwa wakulima na kujumlisha katika ukusanyaji au kuwasiliana na mnunuzi juu ya mahitaji ya ubora, utoaji wa ratiba na kadhalika.

TSS. (Transaction Security Services). TSS ni jina la mchakato ambacho waanzilishi walitumia kujiandikisha, kufuatilia na kukamilisha mikataba ya biashara. Mitandao ya biashara hutumia TSS ‘wazi kitabu’ kama mbinu za biashara zakuwaunganisha wakulima wadogo wadogo na wanunuzi kwa udhibiti wa kutekeleza uwazi na hivyo kupachika uaminifu, kuongeza ufanisi wa soko, kudhibiti hatari na kuongeza thamani kwa wakulima.

Fedha. Biashara zinapewa fedha ili kufidia gharama ya katikati mapema kabla ya kupokea fedha kutoka kwa mnunuzi.