Utangulizi

techfortrade’s imeanzisha huduma inayotoa njia mpya ya kufanya biashara kwa wanunuzi wa mazao ya shamba kwa kuwezesha uwazi na uwajibikaji katika mchakato wa biashara zao.

Kulingana na “Transaction Security Services (TSS)” ulioanzishwa na kampuni ya Rural Africa Investments, huduma hii kubadilisha jukumu la wanabiashara wa mazao ya shamba kwa sababu ni muhimu sana kwa maendeleo ya uhusiano kati ya soko ya wakulima wadogo na wanunuzi wakubwa ambayo imeharibika kwa miaka iliyopita kwa ajili ya kutoaminiana na kukosekana kwa usawa.

Kila hatua ya mpangilio wa biashara unarekodiwa katika kumbukumbu inayotumia mtandao wa internet na hupatikana kwa urahisi kutumia simu ya mkono na kompyuta. Wahusika wote au mtu yeyote anaeza jua kwa uhakika gharama haswa ya katika kila harakati ya kuzinunua mazao zile na bei zinazouzwa.

Tunaamini kuwa njia hii itaweza kujenga imani kwa njia ya uwazi na kuhakikisha ya kwamba wanunuzi na wakulima wadogo watafanya biashara kwa mara nyingine na kuwezesha kupata bei nzuri kwa mkulima na ubora wa mazao kwa mnunuzi. Ya muhimu zaidi ni ya kwamba mtindo huu mpya utabilisha msingi wa haina hii ya biashara kwa maana mfanyabiashara akilipwa kwa muundo tume, itabidi atafute bei nzuri iwezekanavyo kwa mkulima ili naye pia aweze kupata tume nzuri.

Huduma hii inafanya kazi kwa njia gani?

  • Mratibu wa biashara huo anawajibu wa kuweka mikataba kwenye jukwaa letu inayoweka rekodi kwa urahisi na ufanisi zaidi. Jukwaa hili linatumika kwa njia la kuwezesha uwazi na kina katika ukaguzi kwa ajili ya biasharazote zilizofanywa na mfanyabiashara kutumia mbinu hii.
  • Wanunuzi wanaweza kufuatilia mikataba ya kilimo maalum ya asili ili kuhakikisha uwajibikaji na kuzuia migogoro. Kama inahitajika, wanunuzi pia wanaweza kupewa huduma mbalimbali kama ripoti kuhusu biashara yao na kutoa ufahamu wa kina kuhusu gharama zinazohusiana na biashara iyo.
  • Mfanyibiashara anaweza kupata pia fedha za kuwalipa wakulima mapema kupitia mkopo kutoka akaunti inyaoitwa “Cash on the Bag” iliyotekwa kando kwa ajili ya mahitaji kama aya. Fedha hizi zinaweza pia kupewa mapema ili kugharamia gharama zinazohusika na kupanga biashara kama vile usafirishaji na ada zinazolipiwa mpakani.

Huduma hii inalenga wafanyabiashara wa mazao ya shamba na mawakala ambao wanatambua thamani wanaweza kupata katika biashara zao kwa kujenga kuaminiana na wauzaji na wanunuzi. Kwa kuimarisha kuaminiana na uwazi, wanabiashara watazidi kupata kuongezeka kwa mauzaji kati yao na wakulima, na wanunuzi wengine wa mazo ya shamba.

Faida ya huduma hii

Kwa wafanyabiashara:

Huduma hii inatoa fursa ya kipekee ya kugeuza biashara zao kuwa na uwazi, haki na ukweli, na kuwachukilia wakulima na wanunuzi kuwa sawa, kuwapa heshima na kujenga uaminifu mpaka kusababisha kurudia biashara baina yao na kuwa na uhusiano kwa muda mrefu. Kwa kutumia jukwaa hili, wafanyabiashara wataweza kujenga rekodi ya kifedha ya shughuli zao za biashara, kitu ambacho ni muhimu Kwa kuvutia mkopo kutoka kwa benki ya kuwawezesha kupanua na kukua kwa biashara zao. Kwa kulainisha tume ya mfanyabiashara kwa bei ya mkulima, mkulima ataweza kupata bei ya juu na kuhamasisha uhusiano bora na kufanya kazi pamoja kuhakikisha wanapata bei nafuu iwezekanavyo.

Kwa wakulima

Huduma hii inatoa njia salama ya kuuza katika shamba zao na kutoa uwazi kamili na kuelewa halisi gharama wanazozipata wanunuzi wakubwa. Kwa kupatia wananunuzi mkopo kutoka kwa Akaunti ya “Cash on the Bag”, wakullima wanapata kulipwa kwa haraka na kuhakikisha ya kwamba hawatangoja mpaka wakati mnunuzi ameziuza zile bidhaa. Juu ya hayo yote, kama gharama za kusafirisha zile bidhaa ni chini kulikuo ilivyo tarajiwa, au bidhaa zilizo harbika na kidogo kuliko ilivyo tarajiwa, fedha yoyote ya ziada itapewa kwa mkulima.

Kwa wanunuzi

Wale ambao wanatambua haja ya kuongezeka kwa uwazi katika ugavi na kuongezeka kwa hamu ya kuona wakulima wadogo kutendewa haki, kitu ambacho kimekuwa changamoto kubwa mara nyingi wakati wa kufanya biashara kupitia wafanyabiashara na mawakala. Huduma ya techfortrade inatoa njia ya kufikia lengo hili, kutumia urahisi wa chombo kwa ajili ya kufuatilia gharama na bei ya kuhusishwa na kila biashara, kutoka kwa wakulima mpaka kwa ghala ya mnunuzi.

Wasiliana nasi